Usikiaye Maombi

Florence Mureithi

*Usikiaye maombi - Florence Mureithi*

Uhimidiwe Mungu wetu mkuu
Usiyekataa maombi yetu
Usiku na mchana sikio lako li wazi
Unajibu maombi ya wenyehaki

Usikiaye maombi
Kwako binadamu watakuja
Unayejibu maombi
Kwako binadamu watakuja

Una mambo unayo tenda wewe pekee
Ambayo mwanadamu hawezi kamwe
Sikia baba tunapokuita
Dhihirisha nguvu zako tunapoomba

Usikiaye maombi
Kwako binadamu watakujaaa
Unayejibu maombi
Kwako binadamu watakujaaa

Umetuzungushia rehema kama ngao
Kwa wingi wa fathili zako tutakujaaa
Kukusubiri kwa kusali na kuomba
Pasipo kusumbuka na jambo lolote

Usikiaye maombi
Kwako binadamu watakuja
Unayejibu maombi
Kwako binadamu watakuja

Lyrics Submitted by Wanjiku Ngotho

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/