Chorus
Asante bwana kwa wema wako Ooh ooh
Asante bwana kwa pendo lako.*2
Verse 1
Nilipotelea dhambini ukaja kunitafuta,
Ulinikuta gizani ukaniweka nuruni, asante.(Back to chorus)
Verse 2
Nilikuwa mtumwa wa shetani ukaniweka huru,
Nilizama matopeni ukaniosha niwe safi, asante. (Back to chorus)
Verse 3
Bwana umenipa haki kuitwa mwana wa mungu,
Umenipa roho wako awe mwalimu wangu mwema, asante. (Back to chorus)
Verse 4
Bwana nikifika kwako kama ulivyo niahidi,
Nitaimba sifa zako kwa furaha nikisema, asante. (Back to chorus)
Lyrics Submitted by Vincent Chai
Lyrics provided by https://damnlyrics.com/