Moto Umewaka

Angela Chibalonza

Mungu alituma kwangu nguvu zake;
Niwekwe kila saa na neema yake;
Damu ilitoka pamoja na roho
Moto wa upendo unachoma moyo

Moto umewaka, moto umewaka
Moto wa Mungu moyoni umewaka
Roho ameshuka nafurahi sasa
Moto wa Mungu moyoni umewaka.

Mbele ya msalaba, najitoa sasa;
Na niwe saadaka kwa Bwana daima;
Gharama ya dhambi, Yesu alilipa;
Na juu ya sadaka moto unawaka.

Ahadi ya Bwana, sasa naishika;
Kwa neema Yake, nikakubaliwa;
Utukufu wote, ni kwa Bwana Mungu;
Moto wa upendo unawaka kwangu.

Mooto umewaka leo
Mooto ni kazi ya Mungu
Mooto umewaka leo
Tuimbe hallelluya moto umewaka

Watu wote waimbe...moto umewaka
Na wa mama waimbe..moto umewaka
Na wakenya waimbe..moto umewaka

Mooto umewaka leo
Mooto ni kazi ya Mungu
Mooto umewaka leo
Tuimbe hallelluya moto umewaka

Lyrics Submitted by Favour Mwamburi

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/