Ngoja Nicheze

Kwaya Ya Mt.Kizito

NGOJA NICHEZE

@ Bernard Mukasa

Tazama mimi ninavyopumua,
Tazama mimi nilivyo na nguvu *2
Hizo zote - ni neema bure toka kwa Mungu
Na mimi leo - ngoja nicheze muone,
Nitamsifu ngoja nicheze muone,
Bila kuchoka - ngoja nicheze muone aee

Tazama mimi nakula na kushiba,
Tazama mimi nalala nasinzia
Tazama naamka mimi mwenyewe e,
Tazama tazama ah tazama aa aha
Tazama mimi naweza kuongea,
Tazama mimi naimba bila shida
Tazama naweza kucheza mwenyewe e
Tazama tazama ah tazama aa aha
Nikiugua ona napewa pole,
ninapofiwa ndugu mwanifariji
Tazama niwapo na shida wanajaa a
Tazama tazama ah tazama aa aha
Nikikosea huwa nasamehewa,
Nikiudhiwa ndugu mwanitetea
Tazama dhuluma haitaniua a
Tazama tazama ah tazama aa aha
Nikifurahi ndugu washerehekea,
Nikiudhiwa ndugu wasononeka
Tazama ninaishi kati ya watu u
Tazama tazama ah tazama aa aha
Na yote haya najaliwa na Mungu,
Amenipenda upeo wa upendo
Tazama na mimi nitamtukuza a
Tazama tazama ah tazama aa aha

Lyrics Submitted by Evans

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/