Uinuliwe

Upendo Nkone

(Uinuliwe Bwana)
Uinuliwe Mungu muweza
Umeyatenda makuu

Leo tunashangilia
mioyo ina furaha
Yesu umetutendea
Safari ilikuwa ngumu
tulikutana na mengi
yalituvunja moyo
Maneno maneno yalituumiza tukajipa moyo tukamuomba Mungu,
Hatimaye tumevuka
Uinuliwe Bwana aa

Uinuliwe Mungu muweza
Umeyatenda makuu

Yakikupata magumu
Vikwazo vikiinuka
Wewe umuite Yesu
Yeye ndiye anaweza
Tena yeye ana nguvu
Kukufanyia njia
Alisema niite nami nimemuita mwanaume Yesu
amenisikia, na amenipigania
Uinuliwe jemedari

Uinuliwe Mungu muweza
Umeyatenda makuu.

Lyrics Submitted by Melody Makena

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/