Mikononi Mwa Yesu

Penina Musula

MIKONONI MWA YESU

Mikononi mwa Yesu,
Kifuani mwake,
Mapenzi yanilinda,
Sina hofu kamwe;

Ansha tuma wajumbe,
Kuleta habari,
Ya kutufurahisha,
Katika safari;

Mikononi mwa Yesu,
Kifuani mwake,
Mapenzi yanilinda,
Sina hofu kamwe;

Mikononi mwa Yesu
Tashwishi sinayo,
Maonjo hayadhuru,
Madhambi hayamo

Nikiwa na mwokozi,
Sioni majonzi,
Mashaka ni machache,
Machache machozi;

Yesu, mwokozi wangu,
Akafa mtini,
Yesu, mwamba wa kale,
Namtumaini;

Namngojea Bwana,
Mchunga, Rafiki,
Hata kupambauka,
Kule Mashariki

Lyrics Submitted by Thomas Moseti

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/