Uje Unisaidie

Mrs Nancy Torome

UJE UNISAIDIE
Verse 1
Uje unsaidie mwokozi na baraka
Rehema yako ni tele
Najitoa kabisa
Unifundishe kusifu... Sifa za malaika
Umejawa na upendoni upendo wa hakika.

Verse 2
Naja kwako unishike..Najitoa kabisa
Kwa mapenzi yako niwe,mwaminifu wa sifa
Nilipopotea mbali,yesu alinipata
Akaniokoa kweli kwa damu ya salama.

Verse 3
Kwako nimekua mdeni,umenipa rehema
Nisipotele mbali,unifunge kwa wema
Ni mwenye kutangatanga,ni mwenye kupotea
Uchukue moyo wangu,unifunge kwa wema

Lyrics Submitted by Daniel Shirima

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/