Ndoa

Ambwene Mwasongwe

Mlilelewa na wazazi, sasa mmekua
ndio maana mmeamua kuanza maisha yenu.
Mmeaacha baba na mama kuwa mwili mmoja
Ndoa yenu ni takatifu, Mtu asiwatenge
Bila shaka mmejifunza mambo mbali mbali
japokua mmepitia vipindi tofauti.
Katika yote hayo Mshukuruni Mungu x2
kwa kua amewafikisha hapa mlipo x2


Safari yenu ya ndoa, mmeianza kwa imani
ndio maana mwategemea matokeo mazuri.
Yale mtakayotatua mshukuruni Mungu na yatakayowashinda mlilieni pamoja
Imani yenu yote iwekeni kwa Mungu
msiweke katika vitu, shetani asije ona
Akipiga hivyo vitu imani yenu itayumba
Imani yenu ikiyumba nanyi mtayumba
Na ndoa yenu nayo itayumba x2

Neema ikawafunike
yeye Bwana akawe mwalimu wenu
Mungu wenu akawe mshauri wenu

Ndoa ni kama kama jua lenye mwangaza mwanana
Kila lichomozapo wengi hulifurahia
watu makundi makundi hulisifia sana
jua hili jua zuri lina faida kwa afya
Ila jua lilelile likifika mchana,
wengi hulalamika na kulikimbia
Joto likiwazidia wananung'unika x2
Wanasahau walilisifia asubuhi x2


Jua likifika jioni faraja hurejea tena
Ila bahati mbaya jua laenda kuzama
Hapo sifa za asubuhi huanza kusikika upya
walovumilia mchana hula matunda yake
Ila tunawaombea Mungu awatetee
Mtakapofika mchana mkavumiliane
Joto likiwazidia mkasameheane
Msilipize kisasi msije kujidhuru.
Mkakumbuke jioni ya amani yaja x 2


Kama kuna jema lolote msisite kulifanya.
Na neno la Msamaha msilicheleweshe
Mkaishi Maisha yenu, Msiige ya wengine
Epukeni mazoea yanaleta kiburi
Tena maneno mabaya uharibu tabia
kamwe msije thubutu kuyatunza moyoni.
Ndoa ni kipindi cha mwisho cha maisha ya watu
Kitumieni vizuri kwa kua ni kifupi
Maana hamjui lini kifo kitawatenga x2

Mtendee wema mwenzako kadiri utakavyoweza
Moyo unaweza kataa ila jilazimishe
Kama ukitenda wema huna utakachopoteza
Mtendee akiwa hai macho yake yanaona
wengi wanajilaumu kua walikosea
wakati wa kutenda wema wao waliumiza
Mungu akawatenganisha hawaishi pamoja
Wanatamani watende wema ila walichelewa
Maana wenzao hawapo tena x2

Mmeugusa moyo wa Mungu kwa kutimiza agano lake.

Lyrics Submitted by Mpeli M Mwakyeja

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/