Usikumbuke Uovu Wangu

Jane Misso

Usikumbuke uovu wangu Lyrics

Oh Baba nakuja mbele
Oh baba nikumbuke
Oh Baba nimeleta Mambo yangu kwako
Oh Baba nisikilize

Usikumbuke Uovu Wangu mimi
Rehema zako nazihitaji
Nimekutenda uovu nyingi mimi
Nisamehe Baba usikumbuke

Mwana wa Mungu nakuja kwako
Nimesikia habari zako
Unasamehe unatakasa maovu yote Baba
Kwa damu yako Baba nisafishe

Usikumbuke Uovu Wangu mimi
Rehema zako nazihitaji
Nimekutenda uovu nyingi mimi
Nisamehe Baba usikumbuke

Huruma zako zinaniita mimi
Nimesikia mguso wako
Mkono wako Baba wenye uwezo mwingi
Uniongoze Baba kwa nuru yako

Usikumbuke Uovu Wangu mimi
Rehema zako nazihitaji
Nimekutenda uovu mwingi mimi
Nisamehe Baba usikumbuke

Roho wa Mungu chukua leo mimi
Maisha yangu uyatawale
Umefunua uovu wangu mimi
Na mimi leo Baba nibadilishe

Usikumbuke Uovu Wangu mimi
Rehema zako nazihitaji
Nimekutenda uovu mwingi mimi
Nisamehe Baba usikumbuke

Machozi yangu Baba yafute leo
Furaha yangu itimilike
Nisaidie mimi kuendelea mbele
Kusudi lako kwangu litimilike

Usikumbuke Uovu Wangu mimi
Rehema zako nazihitaji
Nimekutenda uovu mwingi mimi
Nisamehe Baba usikumbuke

Song by Jane Misso
Lyrics by Di Camaras

Lyrics Submitted by Di Camaras

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/