Jina

Komando Wa Yesu

Utanieleza nini nisiliamini hili jina?
Linatoa mtu chini linampa heshima
Huu umaskini sio yangu hatima
Japo maumivu si nishukuru kwa uzima
Nitaliamini hata kama leo sina
Mambo ya rohoni wa mwilini hawezi ona
Najua mvua ipo naijenga safina
Japo maumivu najua kesho heshima

Nitaliamini hata kama leo sina
Mambo ya rohoni wa mwilini hawezi ona
Najua mvua ipo naijenga safina
Japo manung'uniko kesho heshima

Ni kweli kila kukicha ni majanga
Ni kweli moyo watangatanga
Naamini yeye aliyepanga
Nipitie haya ana mlango wa kutokea

Sina jina jingine mimi
Ila jina lake eeh
Jina lipitalo majina yote
Yeeeesu

Sina jina jingine mimi
Ila jina lake eeh
Jina lipitalo majina yote
Yeeesu(×2)

Ni kwa jina lake viwete watembea
Ni kwa jina lake vipofu wanaona
Ni kwa jina lake rafiki magonjwa yanaponywa
Huwezi nidanganya eeh

Kwa jina lake tuna ushuhuda
Kwa jina lake vita tunashinda
Na kama ni rafiki ni rafiki wa faida eeh
Huwezi nidanganya mmm

Ni kweli kila kukicha ni majanga
Ni kweli moyo watangatanga
Naamini yeye aliyepanga
Nipitie haya ana mlango wa kutokea



Sina jina jingine mimi
Ila jina lake eeh
Jina lipitalo majina yote
Yeeeesu(×5)

Lyrics Submitted by Charity Maina

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/