Jehanamu Panatisha

AIC Makongoro Vijana Choir

Jehanamu panatisha*4
Jehanamu kuna mateso si kidogo tena usiombe
Jehanamu kuna huzuni ya kutisha haina mfano
Jehanamu kuna upweke wa ajabu tena ni balaa
Jehanamu kuna kilio cha milele

Jehanamu panatisha*4

Baba hakikisha jina lako limeandikwa kitabuni
Mama hakikisha jina lako limeandikwa kitabuni*2

Kitabu kile cha ushindi Kitabu kile cha mbinguni
Kitabu kile cha uzima wa milele
Baba hakikisha jina lako limeandikwa kitabuni

Palikuwa na tajiri aliyekula na kunywa siku zote kwa anasa
Mwenyewe alijiona hapo alipo ameshafika ni hakuna tena*2

Hakumjali mungu hakumjua mungu hakumwogopa mungu hakumweshimu mungu
Alipokufa alipokelewa na dhiki huko kuzimuni

Tena alikuwepo maskini aliyeketi mlangoni pa tajiri
Chakula chake makombo na mwili wake vidonda tupu mbwa walilamba *2

Alimjali mungu alimjua mungu alimwogopa mungu alimweshimu mungu
Alipokufa alipokelewa kifuani pa ibrahimu
Baba hakikisha jina lako limeandikwa kitabuni

Katika kuhangaika tajiri alimwona lazaro akiwa kwenye kifua cha ibrahimu akila mema
Lazaro ametaka vidonda havipo tena Lazaro amenawiri si lazaro wa zamani lazaro amenenepa lazaro anapendeza

Tajiri akiwa kwenye kiu ya kufa alinyenyekea kwa ibrahimu
Baba naomba umtume lazaro anidoneshe tone la maji
Nimrudie baba nahangaika mimi
Nimrudie baba ninateseka sana

Ibrahimu kamjibu tajiri hakika hio itakua ngumu
kwasababu katikati yetu sote tumetenganishwa na jimbo kubwa
yavumilie yote
umeyataka wewe
ulichopanda wewe
ndicho unacho vuna

Sikiliza tajiri alibadilisha maombi yake kwa ibrahimu
lazaro awaambie ndugu zangu duniani wasinifuate mimi
sio pazuri humu
kizazaazaa humu
sio salamaa humu
laana tupu humu

ibrahimu alimjibu tajiri hio nayo haiwezekani
kama mioyo yao ni miigumu ata aende nani hawatasikia ooooohhh

Lyrics Submitted by Sir Sam mualuko

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/