Sina Muda Huo

Jahazi Modern Taarab

Time sina washikaji, wakati sina huu
Na yangu mengi mahitaji sina muda huo
Time sina washikaji, wakati sina huu
Na yangu mengi mahitaji sina muda huo
Mimi naisaka tonge, ili iende vinywani
Sitajitia mazonge kuingia mashakani
Niende huku niende kule kuitafuta riziki
Sio ngumi ila kelele kujiongezea dhiki

Sina muda huo sina
Wa kukaa vibarazani kumdiscussi mtu
Sina muda huo sina
Wa kukaa vipempeni nimsimange mtu
Sina muda huo sina
Wa kukaa vibarazani kumdiscussi mtu
Sina muda huo sina
Wa kukaa vipempeni nimsimange mtu

Na hamu ni zangu, Inanipeleka mbio
Alioniamuru mungu, siyamalizi kwa leo

Iweje ya walimwengu, mie sina muda huo
Msinipikie majungu mie si mke mwenzio
Iweje ya walimwengu, mie sina muda huo
Msinipikie majungu mie si mke mwenzio

Japo sina wa kuchezea naomba maulana nifunguliwe njia
Japo sina wa kuchezea naomba maulana nifunguliwe njia

Kwanza tuheshimiane,
Mimi na we hatushei mume wala huni kunidiscussi
Uwongo tusizuliane,
Na vibaya usiniseme ukanitilia nuksi
Kwanza tuheshimiane,
Mimi na we hatushei mume wala huni kunidiscussi
Uwongo tusizuliane,
Na vibaya usiniseme ukanitilia nuksi

Usitake tuchapane
Me si wewe gumegume
Iliyokujaa mikosi
Ubaya tusitafutane
Kuna kazi si kalime
Kusema usiniforci
Usitake tuchapane
Me si wewe gumegume
Iliyokujaa mikosi
Ubaya tusitafutane
Kuna kazi si kalime
Kusema usiniforci

Hauna haya muone.
Funga domo usiniseme
Niache sina nafasi
Tafuta jambo nyingine
Ila uongo usiseme
Na wajinga usinimissi
Hauna haya muone.
Funga domo usiniseme
Niache sina nafasi
Tafuta jambo nyingine
Ila uongo usiseme
Na wajinga usinimissi

Nina mengi ya kufanya sio kukudiscussi wewe
Tafadhali nakukanya mie sina time na wewe.
Nina mengi ya kufanya sio kukudiscussi wewe
Tafadhali nakukanya mie sina time na wewe.

Sina muda sina muda
Wa kupoteza.
Sina muda sina muda
Wa kudiscussi mtu

Wapi mfalme Mzee Yusufu
Honey, nipapasie kinanda
Niskiie raha

Cha kunishughulisha kwako mie sikijui
Cha kunishughulisha kwako mie sikioni
Cha kunishughulisha kwako mie sikijui
Cha kunishughulisha kwako mie sikioni
Jiangalie juu mpaka chini
Kisha niambie unanisumbua nini
Jiangalie juu mpaka chini
Kisha niambie unanisumbua nini
Hata nikae nikuseme vipembeni
Cha kunishughulisha kwako mie sikijui
Cha kunishughulisha kwako mie sikioni
Cha kunishughulisha kwako mie sikijui
Cha kunishughulisha kwako mie sikioni
Wengi wakuambiwa, kipi usio na macho
Si kikao kukaliwa, Unanini chambilecho
Wengi wakuambiwa, kipi usio na macho
Si kikao kukaliwa, Unanini chambilecho
Muda nililopewa wa kutafuta kinacho
Cha kunishughulisha kwako mie sikijui
Cha kunishughulisha kwako mie sikioni
Cha kunishughulisha kwako mie sikijui
Cha kunishughulisha kwako mie sikioni

Hili lako joto tu hupati baridi maisha yako
Mimi nipo eeh na ntaendelea kuwepo

Mauji mauji, mauji anachana nyuzi
Mauji mauji, mauji anachana nyuzi

Unahamu nikuseme, nikikusema utalia
Unahamu nikuchape, nikukuchapa utazimia
Unahamu nikuseme, nikikusema utalia
Unahamu nikuchape, nikukuchapa utazimia
Unahamu nikuseme, nikikusema utalia
Unahamu nikuchape, nikukuchapa utazimia
Unahamu nikuseme, nikikusema utalia
Unahamu nikuchape, nikukuchapa utazimia

Utabaki ati ati la kwangu hulipati ngo

Lyrics Submitted by Frank Matumaini

Lyrics provided by https://damnlyrics.com/