damnlyrics.com

Abneli

Mbona huyu amefia hapa? Kwanini?

Mbona huyu amenyongwa? Nashangaa

Vyuma vya wageni vimejaa wizi. Kwanini?

Taarifa za habari hakuna mapya. Nashangaa

Huruma, huruma, iko wapi dunia?

Huruma huruma, haipo tena

Huruma, huruma, iko wapi dunia?

Huruma huruma, haipo tenaUsijaribu kumwua nzi aliyekichwani kwa mtu ukatumia nyundo ukidhani unamsaidia

Usijaribu kumwua nzi aliyekichwani kwa mtu ukatumia nyundo ukidhani unamsaidia

Jeraha utaloliacha ni kubwa, ni bora uwaache wenye busara-

Watumie akili wamsaidie

Maana neno msamaha kwa mpumbavu litamwua tu

Ila neno msamaha kwa mwerevu litamwinua

Maana neno msamaha kwa mpumbavu litamwua tu

Ila neno msamaha kwa mwerevu litamwinuaAbneli! Abneli!

Umekufa je Abneli?

Abneli! Abneli!

Daudi alilia

Abneli! Abneli!

Umekufa je Abneli?

Abneli! Abneli!

Daudi alilia

Tumepoteza ndugu zetu, bila sababu

Tumepoteza marafiki, bila sababu

Tumepoteza ndugu zetu, bila sababu

Tumepoteza marafiki, wasio na hatia

Kwa sababu ya kufurahisha, wanadamu

Kwa sababu ya kufurahisha, wanaotuzunguka

Huruma, huruma, iko wapi huruma?

Huruma huruma, haipo tena

Huruma, huruma, iko wapi huruma?

Huruma huruma, haipo tena

Maana neno msamaha kwa mpumbavu litamwua tu

Ila neno msamaha kwa mwerevu litamwinua

Maana moyo wa mwanadamu sasa umekunja ngumi

Roho ya huruma haipo tena

Roho ya kisasi inatenda kazi

Roho ya huruma haipo tena

Roho ya kisasi inatenda kazi

Huruma, huruma, iko wapi dunia?

Huruma huruma, haipo tena

Huruma, huruma, iko wapi dunia?

Huruma huruma, haipo tena

Abneli! Abneli!

Umekufa je Abneli?

Abneli! Abneli!

Daudi alilia

Abneli! Abneli!

Umekufa je Abneli?

Abneli! Abneli!

Daudi aliliaBaada ya Sauli kufa, Abneli alirudi kwa Daudi

Alipotengeneza na Daudi, akasahau Yoabu anakumbuka

Kifo alichomwua nduguye, Asaheli wakati wa vita

Yoabu akamwua Abneli, Abneli hakutambua hilo

Yeye alipotengeneza na Daudi, akajua maadui wamekwisha

Msamaha, msamaha, ukowapi dunia

Msamaha, msamaha, Mungu atusaidie

Msamaha, msamaha, ukowapi dunia

Msamaha, msamaha, Mungu atuhurumie

Nyakati hizi tulizonazo

Alama za nyakati zinaonyesha

Wanadamu wamechoka suru

Wanaona maamuzi kuwa ni kifo

Wajue adui ulio nao

Jihadhari na hao marafiki

Sio kila kicheko kinamaanisha furaha, wengine wakichukia hucheka sana

Sio kila kicheko knaamaanisha upendo, wangene wanataka wakusongeze tu

Wengine wanataka wakuweke karibu, ili iwe sababu ya kutoa roho yakoAbneli! Abneli!

Umekufa je Abneli?

Abneli! Abneli!

Daudi alilia

Abneli! Abneli!

Umekufa je Abneli?

Abneli! Abneli!

Daudi alilia

Song Discussions is protected by U.S. Patent 9401941. Other patents pending.

Enjoy the lyrics !!!