damnlyrics.com

Kama Si Wewe

Kama si wewe Yesu,

singalikua mtu,

lakini kwa upendo wako ulio wa ajabu,

Ulinipa mda wa kutubu dhambi zangu,

Sasa kwa neema yako-o nimeokoka.

CHORUS

Ungalikua binadamu baba,

Ungalisema niuwawe baba,

Kwa zile dhambi zote nimetenda mbele zako,

Lakini baba ulinisubiri nikatambua dhambi zangu zote,

Na nikatubu mbele zako-o nitakuishia (×2).

Nebukadineza alipojiinua

Ulimfanya ale nyasi miaka saba

Ili atambue u-ukuu wako

Lakini alipotubu yeye-e ulimsamehe-e.

CHORUS ×2.

Nakushukuru baba shujaa wa msalaba

Matendo yako baba yanisukuma kukuabudu

Hata nikinyamazishwa wala Mimi sinyamazi

Umeniokoa bure Yesu-e nakushu-ku-u-ru.

CHORUS ×2.

Lyrics Submitted by Jeinny

Enjoy the lyrics !!!