damnlyrics.com

Kiboko Yangu

kwa sifa moja umenikamata, nakupa

we peke yako ndo umeniweza... heey

nilikopita nimeteleza, lakini kwako

we ndio kiboko yangu

kila shetani ana mbuyu, wake we ni mibuyu mitatu

ukiamua unitumikishe mwenzio ntalala na viatu

najionea maajabu najionea mapya mama 'angu

hakuna mapenzi ya hivi popote kwenye ulimwengu

siwezi elezea jinsi ninavyokuzimia

nikicheza na moyo wako nacheza na wangu pia

nafsi yangu ilishapotea siwezi hata kujitetea

ka' ulitoroka peponi uzuri ulivyokuenea

figure la kushoto ntageuza na la kulia

wengine hawanijaribu wanajua kitachotokea

sitaki mambo yaende kombo, na yakienda yawahi kurudi

hatuendi nayo hatuwezi shindwa yaje na pambio ikibidi

tunapishana hatugombani, then we back here

hatuendi juu hatuendi chini ila we love it right here

hata mapenzi yakifa boo situbaki sawa tu

si' ni watu wazima halafu hatuwezi ishi ka' underground

ukiwa na nusu ya moyo wangu na nusu iliyobaki kwangu

yote nakupenda wewe, una Jua langu na mwezi wangu

unatembea na roho yangu, sio tena .......

we ndio Michelle Obama wangu

kwa sifa moja umenikamata, umenikamata!

we peke yako ndo umeniweza... umeniweza!

nilikopita nimeteleza, lakini kwako

we ndio kiboko yangu

sipagawi, hawajui kwanza

we ndio namba moja unawakimbiza

unatembea na roho, nataka ujue

wewe ndio kiboko yangu

Lyrics Submitted by Meeknego

Enjoy the lyrics !!!