damnlyrics.com

Kidudu Mtu (feat. Baby J)

(opening conversation)

Kina dada mpo?

Eeg, mambo

Shwari

Upo wewe? Niambie

Habari

Ipi tena?

Una habari wewe?

Ipi?

Wala si nyeupe, kina...

Wan'fanya nini?

Wanakuloga shoga'angu

Wanakuloga

Ulijuaje kama wewe sio mchawi

Ulijuaje na kama wewe sio mchawi?

Wanakuloga...

Haiya haiya kidudu mtu

Haiya haiya kidudu mtu

Unafitinisha wenzako we hujali utu

Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie

Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie

(Offside)

Kidudu kidudu gani usie tulia

Una maneno machafu watupakazia

Kidudu kidudu gani usie tulia

Una maneno machafu watupakazia

Imefika siku yako yaku simuliwa

Maisha yako ya nyuma yalipoanziaaa

(Baby J)

Acha usutwe sutwe hujakoma wewe kidudu mtu

Yako yanakushinda ni hodari tu kusema ya watu

Hizo ni sifa mbaya jali utu wewe kuliko kitu

Hutoishi na watu roho yako chafu safisha kutu

Haiya haiya kidudu mtu

Haiya haiya kidudu mtu

Unafitinisha wenzako we hujali utu

Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie

Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie

(Offside)

Ulikuja kwa uzuri tukakupokea

Tukakuona wa maana kumbe ni mmbea

Ulikuja kwa uzuri tukakupokea

Tukakuona wa maana kumbe ni mmbea

Mimi ni kama bahari ukinichafua

Nadondosha meli kubwa seuze ngarawa

Haiya haiya kidudu mtu

Haiya haiya kidudu mtu

Unafitinisha wenzako we hujali utu

Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie

Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie

Hapo! Hapo!

Hapo! Hapo!

(MPASHO)

Offside Trick watoto wa ki-Zanzibari wakali wa hizi kazi

Umeskia wapi superstar anakula kwa mama ntilie?

Superstar anakula Kempinski bwana! Utafungwa

Wape vidonge vyao dada

Jamani eee!

Maisha ni kutafuta na sio kutafutana babu ee

Wenzako wanaomba kazi wewe waomba pesa

Asiohaya wala hajui vibaya

Mvalisheni dira sasa pamoja na chupi la bambino hei!

Yako hilo babu!

Watakuchum' babu mmm-mmwah

Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho

Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio

Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho

Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio

Hapo! Hapo!

Hapo! Hapo!

Hapo! Hapo!

Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho

Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio

Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho

Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio

Lyrics Submitted by Majini ya Mombasa

Enjoy the lyrics !!!