damnlyrics.com

Kutakuwa Mwanga

Kutakuwa Mwanga

Kutakuwa mwanga nyumbani mwa Bwana,

Nifikapo mwisho wa mwendo;

Nitapata raha mkononi mwa Bwana,

Nifikapo mwisho wa mwendo.

Safari ikomapo siku ya mwisho,

Nitakaribishwa na pendo;

Kwa kuwa Mwokozi ananingojea,

Nifikapo mwisho wa mwendo.

Sitazikumbuka taabu za njiani,

Nifikapo mwisho wa mwendo;

Sitawakumbuka walionipinga,

Nifikapo mwisho wa mwendo.

Nimwone rafiki aliye Mwokozi,

Nifikipo mwisho wa mwendo;

Hivyo natamani katika mbinguni,

Nifikapo mwisho wa mwendo.

Lyrics Submitted by Wapang'ana Abraham

Enjoy the lyrics !!!