damnlyrics.com

Mbele Ninaendelea

MBELE NINAENDELEA

1. Mbele ninaendelea ninazidi, kutembea

maombi uyasikie, Ee Bwana unipandishe.

Ee Bwana uniinue, Kwa imani nisimame,

Nipande milima yote ,Ee Bwana unipandishe .

2.Sina tamani nikae, mahali, pa shaka kamwe,

Hapo wengi wanakaa , kuendelea naomba

3.Nisikae duniani, ni mahali pa shetani,

Natazamia mbinguni, aitafika kwa imani

4.Nataka nipandishwe, juu zaidi yale mawingu,

Nitaomba nifikishe, Ee Bwana unipandishe.

Lyrics Submitted by MERED DENNIS

Enjoy the lyrics !!!