damnlyrics.com

Mteule Uwe Macho

Mteule Uwe Macho – Rose Muhando

1. Ooh ye dunia sasa imashakani

Kumbe dhambi imekuwa kitu cha kushangiliwa

Makala makubwa imejengewa ngome za kifahari

Ooh ye dunia sasa imashakani

Kumbe dhambi imekuwa kitu cha kushangiliwa

Makala makubwa imejengewa ngome za kifahari

Mabomu ya kujitoa muhanga ni jambo la hatari

Wakati damu hiyo hatia ni jambo la kutisha

Yaliyonenwa na nabii Danieli sasa yanatimia

Ni nani atasimama, mbele ya hasira ya Bwana

Atulize ghadhabu yake isiipate dunia

Ni nani atasimama, mbele ya hasira ya Bwana

Atulize ghadhabu yake isiipate dunia

Eeeh, lelelelelelele

Mteule uwe maaaacho

Ni siku za mwisho nasema

Chorus:

Mteule uwe macho, hizi ni siku za mwisho

Kwani yale yaliyotabiriwa sasa yanatimia

Tusimame imara tujifungeni miganda

kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele

Mpigeni shetani, mnyang’anye mamlaka

Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni

Uwe macho, hizi ni siku za mwisho

Kwani yale yaliyotabiriwa sasa yanatimia

Tusimame imara tujifungeni miganda

kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele

Mpingeni shetani, mnyang’anye mamlaka

Tupilia mbali tamaa ya dhambi, Weka pembeni

2. Kutangatanga kwako wewe, mbona kwa kuchelewesha

Nachelewa kusema nawe, utafuna ulichopanda

Shika sana ulicho nacho, Yesu yu karibu kucha

Mwenye sikio asikie, roho asema na kanisa

Eeeh, lelelelelelele

Ah yayayayaya

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Muongo endelea kutenda dhambi, dunia ikujuee

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Mumbea endelea kusema umbea, vunja nyumba za watu

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Mchawi endelea kuroga sana, mchana wewee

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

3. Wachungaji tuelezeni, mwatupeleka wapi jamani

Mbona bishopu mwanamume, ameoa mume mwenzie

Andiko hili latoka wapi, tena kwenye Bibilia gani

Watoto wetu wa kiume, tuwafiche wapi jamani

Wamama nao bila aibu, wazini na vijana wadogo

Sasa tutapataje kupona, ukimwi utatumaliza

Eeeh, lelelelelelele

Ah yayayayaya

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Kahaba endelea kufanya ukahaba, mpaka kwenye internet

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Malaya endelea kufanya umalaya, utakwenda na bomu

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Washerati endelea kufanya dhambi, Yesu yuaja

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Lokole endelea kujitakaza, Yesu yuaja

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Shoga endelea kufanya ushoga, mpaka kwenye mtandao

(Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi)

Eeeh, lelelelele

Jamani nasema

Chorus:

Mteule uwe macho, hizi ni siku za mwisho

Kwani yale yaliyotabiriwa sasa, yanatimia

Tusimame imara, tujifungeni miganda

kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele

Mpigeni shetani, mnyang’anye mamlaka

Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni

Uwe macho

Oh, yeyeye, yeyeye

Oh yeyeyeye

Uh yeyeyeyeye

Lyrics Submitted by Dennis Mulongo

Enjoy the lyrics !!!