damnlyrics.com

Nilikuwa Msafiri

Nilikuwa msafiri bora, wa kwenda mbinguni,

Nilikuwa nao wenzangu tukipeana moyo.

Nilipofikia karibu, ya kuvuka ng'ambo,

Nikajawa kiburi, cha ushindi, bila kutambua.

Nika anza kurudi nyuma, nikayarudia matope,

Niliokuwa nao wote wakaniacha.

Chorus

Mi nifanye nini...

Njoo Kwa Yesu, X2

Bado muda mfupi Kwa anaye taka toba,

Niende wapi...

Anza safari,

Siwezi tena...

Usife moyo, shujaa wa msalaba Yuko mbele akuita.

Ng'ang'ania wokovu taji inakungoja. X2

Nimatendo mengi maovu, niliyoyatenda,

Nimesha mkosea Mungu aliyenikomboa,

Nina wasiwasi ya kwamba, sitapokelewa,

Nimepoteza dira, ya wokovu, nita angamia,

Nani atanisaidia, anitoe Mimi shimoni,

Nisiangamie na dunia hii ya dhambi.

Chorus

Mi nifanye nini...

Njoo Kwa Yesu, X2

Bado muda mfupi Kwa anaye taka toba,

Niende wapi...

Anza safari,

Mi Siwezi tena...

Usife moyo, shujaa wa msalaba Yuko mbele akuita.

Ng'ang'ania wokovu taji inakungoja. X2

Sasa nimejua ya kwamba, kuwa mbali sana,

Sio chanzo changu Mimi kukataliwa na Yesu,

Na sasa naanza Safari, ya kumfuata Yesu,

Nitaung'ang'ania, msalaba, Hadi nifike juu, (mbinguni).

Sitaki rudi nyuma tena, nimesha amini ya kwamba,

Wokovu umeandaliwa kwa ajili yangu.

Chorus

Mi narudi Kwa Yesu...

Njoo Kwa Yesu, X2

Bado muda mfupi Kwa anaye taka toba,

Naanza Safari...

Anza safari,

Mimi tasonga mbele...

Usife moyo, shujaa wa msalaba Yuko mbele akuita.

Ng'ang'ania wokovu taji inakungoja. X3

Lyrics Submitted by Jesse Nyimba

Enjoy the lyrics !!!