damnlyrics.com

Nimezama Kwa Mapenzi

Nimezama kwa maapenzi,sijui kama nitazuka

Naiona yangu hali ,mimi nimedhoofika

Nimezama kwa mapenzi , sijui kama matazuka

Wenzangu nawauliza , nini dawa ya mapenzi

Waganga nimemaliza , kwa makombe na hirizi

Ilaahii mola muweza ,ataniaafu mwenyeezi

Nimezama kwa mapenzi , sijui kama matazuka.

Nimezam kwa mapenzi , sijui kama atazuka

Kujikwamua siwezi , taabani nateseeka

Ilaahi mola mwenyezi, ataniaafu rabuuka.

Nimezama nimezama, mwenzeenu katika kina

Mwenzenu katika kina , nimebaki natizama

Kwa kupenda sina tena, ilaahi mola kariima

Ataniaafu rabaana.

Nimezam nimezama, katika kina kireefu

Kila nikijitizama, moyoni napata khofu

Ilaahi mola karima, ndiyo mwenye kuniaafu.

Nimezama nimezama kwenye bahari ya huba

Moyo wangu walalama, ndani yakiti ako

Ilaahi mola karima, ataniepushia adhaba.

Naionq yangu hali, mimi nimedhoofika

Nimezam kwa mapenzi , sijui kama atazuka

Nimezama kwa mapenzi , sijui kama atazuka..

Lyrics Submitted by Idd mussa

Enjoy the lyrics !!!