damnlyrics.com

Nitawapumzisha

Njooni kwangu nyinyi nyote ,msumbukao na mizigo mizito

msifadhaike nitawapumzisha,Nira yangu ni laaini

mzigo wangu ni mwepesi mno

jifundusheni kwangu mimi ni mpole .

Njooni mlio vunjika mioyo

njooni wenye mioyo mizito

nitawaganga niwaponya

nitawapa furaha,

mimi ni baba wa yatima ,

njooni nyote mnaolia,

niwajaza na roho wangu nitawafariji

Msiogope kwa sababu ,nyinyi ni bora kuliko kondoo

mmewashinda mashomoro sitawasahau

Nimesikia kilio chenu nitayavuta machozi yenu yote

nitawashika mikono nitawasaidia

Tafuteni ufalme wangu, utafuteni uso wangu

nitawajaza kila mnacho hitaji

njooni kwangu maskini nitawapa utajiri wangu

njooni wenye dhambi nitawaokoa

Lyrics Submitted by kenneth Micheni Duncan

Enjoy the lyrics !!!