damnlyrics.com

Nitume Mimi Bwana

K /:nitume niende,nitume nikwande

Duniani kote,kuhubiri neno lako

Bwana unitume,ewe Bwana unitume:/

1. Eeh mungu Naitika wito wako

Umenijua mimi hata kabla sijaumbwa kabla

sijazaliwa mimi wewe uliinitakasa,

Bwana toka tumboni MWA mama yangu

Ukanifanya kuwa nabii na mtumishi wako Niko

tayari eeh mungu.

2. Unitie nguvu na ushupavu

Nisimamie ukweli na kutetea Imani

Tena niimarishe mimi ni hubiri neno lako

Mimi ni mtumishi wa bwana

Na nitendewe ulivyo nena na naja

kufanya mapenzi yako Niko tayari eeh mungu

3. Nijalie na roho mtakatifu

Aniongoze katika utume wangu

Mimi nidumu mile daima katika kukutumikia

Bwana nitume mimi kutangaza

Mwaka wa bwana kuwahubiri maskini

Habari njema Niko tayari eeh mungu.

Lyrics Submitted by Ephantus muiruri

Enjoy the lyrics !!!