damnlyrics.com

SHE GOT A GWAN

Tukianzia uzuri tu she got a gwan

Tabia, heshima ndio duu, she got a gwan

Mpaka kwa masista duu yeah

Nabaki tu kusema uh she got a gwan

Mara ya kwanza mi namuona East Zoo, Dodoma

Ghafla nakajihisi kama mtu mwenye homa

Kutoa salamu tu jibu lake ni noma

Sauti yake tu nkajihisi nimepona

Ndefu yake shingo, mwendo wa maringo

Nilifurahi aliponiambia yuko single

Sio siri mtoto huyu ameumbika

Na kama akipita mbele ya watu kumi basi

Nane kati yao lazima watababaika

Hata hao wawili wivu tu umewashika

Kila saa kwa Ngwair ndo amefika

Nami naapa kamwe sintomuacha

Mi naimani atanizalia mapacha

Na hata kama bahati mbaya akiwa tasa

Mnajua sitoweza kumuacha

Na yote ni sababu tu she got a gwan

Tukianzia uzuri tu she got a gwan

Tabia, heshima ndio duu, she got a gwan

Mpaka kwa masista duu yeah

Nabaki tu kusema uh she got a gwan

Sitosahau mara ya kwanza ameniruhusu

Nimbusu, nitomase zake chuchu

Naona fahari leo mpenzi uko na mimi

Na ninaahidi milele ntakuthamini

Sitojali ashatembea na wangapi

Kuwa nawe maishani naona bahati

Kila unapopita masela unawadatisha

Babaisha, wanabaki macho juu juu

Wakuonapo maduu wanakasirika

Kunja ndita, wanabenua midomo juu

Najua yote hiyo ni wivu tu

Washakuzushia mambo mengi tu

Ila wewe ndio my baby girl, mmoja wa pekee

Siwezi kuwa na raha bila kuwa na wee

Na kosa naomba unisamehe

Nataka kuwa na wewe milele, okay, you got a gwan

Tukianzia uzuri tu she got a gwan

Tabia, heshima ndio duu, she got a gwan

Mpaka kwa masista duu yeah

Nabaki tu kusema uh she got a gwan

Nionyeshe ulichonacho maa

Nionyeshe zaidi ya nguo zako ulizovaa

Nionyeshe zaidi ya ngozi yako ya kung'aa

Nionyeshe kile ambacho kitanipa raha (hey hey hey)

Girl, you got a gwan

You're my number one

And nia yangu mi ni kuwa nawe maishani

Chochote unachotaka mi ntakupa weka imani

Na mi naahidi kamwe wala sitokuacha njiani

She got a gwan!

Yes, I know

Mama get busy, twende kwenye dance floor

Unapokata kiuno matozi wanapagawa

Utasikia sauti zao wakisema "yeah, yeah, yeah"

Na atakae shobokea mi ntamtoa dunia

Na kuanzia leo ntakuwa natembea mi na gun (ooh)

Naona milupo imeanza kuntamani

Basi malizia kinywaji twende zetu nyumbani

Girl!

Tukianzia uzuri tu she got a gwan

Tabia, heshima ndio duu, she got a gwan

Mpaka kwa masista duu yeah

Nabaki tu kusema uh she got a gwan

She got a gwan

Girl, you got a gwan

Uzuri kuwa na wewe sio siri naona furaha

You got a gwan

Girl, you got a gwan

Oh baby wewe ndo my number one

Number one, number one

You're the one

Lyrics Submitted by Kanungila Karim

Enjoy the lyrics !!!