TAIFA TEULE
Taifa teule Israeli walimuasi Bwana
Wayahudi nao wakafanya mbinu zakumuuwa
Waka mukamata wakamubeba mbele ya Pilato
Kwenye askar iwa kirumi katili kama Goliati
Pilato kauliza mwataka nimfungulie nani
Wakasema wote mfungulie mupora Baraba
Nimtende je Yesu, wakajibu huyo msulubishe
Damu yake huyo iwe juu yetu na watoto wetu
Yesu akawatazama kwa huzuni
Ai ya iya iya –
Ndipo katolewa ili apigwe na kuteswa sana
Kikosi kizima kama kondoo aendaye kuchinjwa
Kavuliwa nguo, kapigwa kwa mijeledi ya ngozi
Ngozi zenye ndoano zikauchubua mwili mzima
Taji ya miiba wakaigonga kwa nyundo kichwani
Hakutamanika, walimjaza mate ya usoni
Tukimtazama anavuja damu mwili mzima
Bado msalaba unamngoje ili aubebe
Yesu akasema Baba wasamehe
Aiya iya iye eh –
Yesu kauliza Israeli mbona waniumiza
Nimekuja kwenu ili niwaleteye ukombozi
Kila nilipopita nimewatendea mema ninyi
Mumenikamata kwa sababu nimetenda mema
Nimekaa kwenu na wagonjwa wenu nimewaponya
Walio pooza hata wafu wenu nimefufuwa
Vipofu wenu wameona, chakula nimewalisha
Nani kati yenu anaye nishuhudia dhambi
Nimekuja kwa watu wangu, mmenikataa eh
Asikari warumi wakamtwika msalaba wake
Umejaa dhambi za watu wote wa dunia hii
Hebu mtazame mwana wa Mungu alivyo umizwa
Walivyo muweka msalabani bila ya mavazi
Mikono miguu imeshikiliwa na misumari
Wakampa siki, wakamchoma mkuki ubavuni
Machozi na damu na maji vilifanya miferegi
Hakufarijiwa, hata jambazi alimtukana
Wanawake walimlilia kwa huzuni
Aiya iya iya ah –
Mungu katazama, kaona mwanaye kajaa dhambi
Akatanda giza, hakutamani kumuangalia
Yesu kainua macho yake asimwone babaye
Akalia sana Baba yangu mbona umeniacha
Kilio cha Mwana kikajaa mbingu wote uzuni
Mungu kakumbuka mwanangu ni mimi nilimtoa
Akajifunua, ndipo Yesu kasema imekwisha
Mikononi mwako Baba ninaiweka roho yango
Yesu akainama kakata roho aiya iya iya oh –
Yesu kauliza mwanadamu mbona mwaniumiza
Nimekuja kwenu kusudi niwaletee uzima
Kila nilipopita nimewatendea mema ninyi
Mmenikamata kwa sababu mimi naokoa
Nimekaa kwenu na wagonjwa wenu nimewaponya
Waliopooza hata wafu wenu nimefufuwa
Vipofu wenu wameona, chakula nimewalisha
Nani kati yenu anaye nishuhudia dhambi
Nimekuja kwa watu wangu mmenikataa eh
Yesu aliumizwa…
Lyrics Submitted by Dieumerci