Unijaze Roho nifurike,
Ninahamu ya mguzo wako.
Mungu wangu niko hapa mbele zako,
Nikwabudu ,nishujudu,nikuinue,
Nainua macho yangu kwako mbinguni,
Huko ndiko nguvu zangu zinakotoka,
Peke yako Baba yangu nakutukuza,
Nguvu zote mamlaka ni vyako wewe.
Ewe Roho Mtakatifu ninaona kiu,
Kama ayala atamanivyo mito ya maji,
Ndivyo name moyo wangu unakutamani,
Ishi kwangu ndani yangu unitie nguvu
Mwaimu mwema ninaomba unifundishe,
Unioshe,unichunge unibadilishe.
Uje kwangu ewe Roho unitakaze,
Moyo wangu na matendo nimpendeze Yesu,
Unijaze kama siku ya Pentekoste,
Walijazwa wakanena kwa lugha mpya,
Kaa name siku zote unielekeze,
Yesu wangu uniponye,
Unipe Amani.
Enjoy the lyrics !!!