damnlyrics.com

Alipofika Karibu Aliona Mti

ALIPOFIKA KARIBU ALIUONA MJI - Ulyankulu Barabara 13

1.Alipofika karibu aliuona mji

Akaulilia akisema

Alipofika karibu aliuona mji

Akaulilia akisema

(Laiti),

Ungalijua hata wewe

(Katika),

Siku hii yakupasayo amani

(Laiti),

Ungalijua hata wewe

(Katika),

Siku hii yakupasayo amani

2.Lakini sasa yamefichwa machoni pako

Kwa kuwa siku zitakuja adui zako

Lakini sasa yamefichwa machoni pako

Kwa kuwa siku zitakuja adui zako

(Wata),

'pokujengea boma likuzunguke

Watakuzingira kukuhusuru pande zote

(Wata),

'pokujengea boma likuzunguke

Watakuzingira kukuhusuru pande zote

(Wata),

kuangusha chini wewe na watoto wako

Wasikuachie jiwe juu ya jiwe

Kwasababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako

(Wata),

kuangusha chini wewe na watoto wako

Wasikuachie jiwe juu ya jiwe

Kwasababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako

3.Watu wa Yerusalemu walitenda maovu

Wakamchukiza muumba wao

Watu wa kizazi hiki wametenda maovu

Wamemchukiza muumba wao

Watu wa Yerusalemu walitenda maovu

Wakamchukiza muumba wao

Watu wa kizazi hiki wametenda maovu

Wamemchukiza muumba wao

(Yesu),

Anaililia dunia ya leo

(Yesu),

Anawalilia watu wa leo

Wametenda dhambi kupindukia

Wamemchukiza muumba wao

(Yesu),

Anaililia dunia ya leo

(Yesu),

Anawalilia watu wa leo

Wametenda dhambi kupindukia

Wamemchukiza muumba wao

(Laiti),

Ungalijua hata wewe

(Katika),

Siku hii yakupasayo amani

(Laiti),

Ungalijua hata wewe

(Katika),

Siku hii yakupasayo amani

Njoo, Njoo, Njoo, Njoo!

Kwake Yesu usamehewe

Kwake Yesu utakasike

Kwake Yesu utapona

Siku moja utaingia mbinguni

Kwake Yesu usamehewe

Kwake Yesu utakasike

Kwake Yesu utapona

Siku moja utaingia mbinguni

Njoo, Njoo, Njoo, Njoo!

Kwake Yesu usamehewe

Kwake Yesu utakasike

Kwake Yesu utapona

Siku moja utaingia mbinguni.

Lyrics Submitted by Martin

Enjoy the lyrics !!!