Dar mpaka moro - TMK Wanaume
| Page format: |
Dar mpaka moro Lyrics
Haayaaaaaa!
Haaaayaaaaa!
Mshikaji wangu YP skiaa
Kuna mtoto mmoja nimemzimiaa
Anasema nimfuate Moro,
Kule wanakotoka Wapogoro
Yepo Nina sije, yeponi na sije
Tukimfuata tutaonekana wadhaifu!
Wee unaonaje, wee unachukuliaje
Kama vipi mtoto hatoshuka Dar?
Anasema kuja Dar hatoweza
Kwa nini??
Anahofia wazazi kumgombeza
Hiyo yote sababu yupo skuli
Akimaliza mbona itakua shwari
Usijifanye una uhakika wee Chege
Isije ikaonekana si ni mabwege
Labda twajichanganya
Na sisi hatuna kitu itakuaje?
Mtoto mambo safi kwao kuna noti
Kwenye shavu,noma cheki mtoto blue band
Mtoto safi kwenye friji kila kitu hakikosi
Figa nayo freshi ukicheki mikosi
Bas kama vipi basi chege twende Moro
Haaayaaaa!
Haina noma YP bas twende Moro
Haaayaaaa!
Chorus
Hamna noma baby nitakuja Moro
Nisubiri kwanza niongee na masela
Kama kunaendeka nijue, kama hakwendeki nijue
Wapi? Dar mpaka Moro x2
Kuna nini wanangu?
Na nyie kwa akili sio siri mmekithiri
Juzi mlikua Mbeya, Jana mkaenda Iringa
Leo tena twende Moro, kuna ninii? Mmh!
Haina noma kule kila kitu mwake
Hakuna shida vinywaji lazima update
Kila kitu mwake
Nauli iko wapi
Mi hapa sina hata bati
Na kutafutia wapi
Sio kama sitaki eeh
Kule kila kitu safi kuhusu kesho
Naona tunachelewa tufanye upesi
Ah Sio kihivo sio kihivo wewe
Hamnitoi hapa kiurahisi
Japo Moro nimepamisi
Sio kama nawadisi
Nyi mnacheza na madem was SKU izi
Mtapigwa changa kwa huo mwendo wenu wa kujimwaga
Mtachezewa mchezo muone dunia ngumu
Haki ya mungu
Msione wamependeza
Wamebugia vya dunia
Mtakuja kujutia eh
Mi mi mi mi mi simo!!
Chorus x2