damnlyrics.com

Kando Ya Mto

1.Kando ya mto ndipo tulipo keti

Tukikumbuka nyumbani Yerusalemi

Tukasikia amri ikitolewa kwetu

Tuimbe ,wimbo wa Bwana nchi ya ugenini

CHORUS

Tungewezaje kuimba wimbo wa Bwana huko

Tukitetea imani uko ugenini

(Na leo-Bass) wanatafutwa watakao tetea (ooh tetea)

Imani ulimwenguni wakimukiri Bwana

2.Kama mitume wengi walisimama

Wakitetea imani hata mauti

Wakisema wazi wazi heri Kufa na Yesu (ooh Yesu-tenor)

Kuliko raha kitambo wewe wasemaje

Lyrics Submitted by Ruth Omwanza

Enjoy the lyrics !!!