damnlyrics.com

Karibu Na Wewe

Karibu na wewe, Mungu wangu

Karibu zaidi, Bwana wangu

Siku zote niwe karibu na wewe

Karibu zaidi, Mungu wangu.

Mimi nasafiri duniani, pa kupumzika sipaoni,

Nilalapo niwe karibu na wewe

Karibu zaidi, Mungu wangu.

Yote unipayo yanivuta, pa kukaribia nitapata,

Na nielekezwe karibu na wewe

Karibu zaidi, Mungu wangu.

Na kwa nguvu zangu, nikusifu

Mwamba uwe maji ya wokovu

Mashakani niwe, karibu na wewe

Karibu zaidi, Mungu wangu.

Na nyumbani mwa juu, Baba yangu

Nikinyakuliwa toka huko

Kwa furaha niwe, pamoja na wewe

Karibu zaidi, Mungu wangu.

Lyrics Submitted by Silas Nyachae

Enjoy the lyrics !!!