damnlyrics.com

Kukataliwa Ni Kubaya

Kama kweli kukataliwa jamani kubaya sana

Nasitukia nimebaki kuzubaa nisijue la kufanya oooh!

Nimejinamia kama ng'ombe anayekula majani

Butwaa limenishika masikio hayafanyi kazi. oooh!

Jama wanavyonisemesha naona kama picha .

Lakini mawazo na fahamu, pale pale sina. Oooh!

Mapenzi yakikushika kumbe akili hurika.

Kama umefiwa na baba na mama siku moja. Oooh!

Natamani kula sumu..............

Lakini nakumbuka watoto wangu watabaki na nani. Oooh!

Lyrics Submitted by Kenyatta mong'are

Enjoy the lyrics !!!