Kula Neno - Rosemary Njage
Page format: |
Kula Neno Lyrics
KULA NENO BY ROSEMARY NJAGE
VERSE 1
Tunaolifahamu, neno lako Baba, hatutatingizwa na jambo lolote.
Tunaokula, neno lako.. Baba ...baba... babaaaa....
Sisi ni tofauti, na watu wengine.
Shetani akileta magonjwa, tunasimama wima.
Twamtangazia kwa mapigo, ya Yesu tumepona.
Wachawi wakituroga, wala haturogeki
Uchawi wao wayeyuka, mbele ya macho yao.
Maana tumekula neno, hakuna silaha yoyote,
Itakayo faulu, kinyume chetu sisi
CHORUS :
Nitakula neno,
Nutakula neno lako Baba
Maana neno lako, ni yote juu ya yote.
Nitakula neno,
Nitakula neno lako Baba
Maana neno lako limedhibitika.
(×2)
VERSE 2
Tunaolifahamu neno lako Baba,
Tutamiliki manyumba tusiyoyajenga
Neno lako pia, tutakanyanga nzige na nyoka
Wala hawatatudhuru, maana tumekula neno
Mafundisho ya uongo, yakichanganya watu,
Sisi tumekula neno, hayatuchanganya
Yeremiah akasema, niliposoma neno lako Baba
Nami nikayala, yakawa furaha kwangu
Furaha tuliyo nayo,
Maana twalifahamu neno,
Na tumeitwa kwa jina la Bwana wa majeshi.
CHORUS :
Nitakula neno,
Nutakula neno lako Baba
Maana neno lako, ni yote juu ya yote.
Nitakula neno,
Nitakula neno lako Baba
Maana neno lako limedhibitika.
(×3)
Lyrics Submitted by Jackline Watahi