DamnLyrics - The center provides all the lyrics


     
Page format: Left Center Right
Direct link:
BB code:
Embed:

Mpeni Kaisari Lyrics


MPENI KAISARI
Vipaji tumepewa, mapato tumepata
Lakini binadamu tunashindwa kushukuru
Wakati tunaomba, tunajinyenyekesha
Lakini tukipata mikono yetu birika
Mpeni kaisari, yaliyo yake
Mpeni Mungu (yale) yaliyo yake Mungu *2
Mifugo tunafuga, nafaka tunavuna
Lakini kila siku tunakula na kusaza
Kumbuka kuna wale, wasio na chochote
Hawawezi kupata, hata kikombe cha chai
Tunapofanya kazi, twapata mishahara
Shughuli zetu sisi kuingia kwenye baa
Ikiwa zitabaki, twakuja kanisani

Twamtolea Mungu, shilingi moja na tano
Tukiwa na wagonjwa hatuwasaidii
Wakati wamekufa tunachanga kwa huzuni
Twachukua mikopo, kwa mambo ya anasa
Ujenzi wa kanisa, twalazimishwa kutoa.
Kumbuka Ibrahimu, alitoa mwanawe
Kama sadaka kwake Mungu Baba wa mbinguni
Na sisi kwa furaha, tupeleke zawadi
Itakayopendeza, kama ile ya Abeli
Lyrics Submitted by Haron Muriithi

Enjoy the lyrics !!!