damnlyrics.com

Saa Heri Ya Maombi

1. Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,

Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu.

Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,

Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.

2. Saa heri ya maombi, Twapeleka dhiki zetu

Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.

Huagiza tumwendee, tutegemee Neno lake,

Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.

3. Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia

Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.

Yesu atatusikia, tutamtafuta daima,

Na tutakapokutana tutamwona-saa tamu!

Lyrics Submitted by Rev Samuel Githinji

Enjoy the lyrics !!!