damnlyrics.com

Utajiju

Haya tena lile kundi lako kubwa kabisa la bongo record (records)

linakuletea tamasha zuri kabisa la mziki wa hip hop

ambalo linaletwa kwenu na msanii Juma Nature

atawarusha kinona kwa kiingilio cha shilingi elfu mbili

VERSE (JUMA NATURE)

Anatokea jamaa sijui anautaira gani

Kwani kiingilio shingapi mbona mnanichefua chefua

Tunakuchefua nini kwani ujasikia buku mbili

Sasa hiyo buku mbili si bora nikanune ubwabwa tu

Mzee starehe gharama na mziki unawatu wake

Kama pesa yako ndogo nenda tu ukanune maziwa

Uiondoe hiyo sumu yako ya maneno yako machafu

Uwaache wenye ela zao wajichane waburudike

Usivamie usivyoviweza dunia itakuadhibu hii

Sio fresh kumaind misala

Tangaza live ili tujue usionge tu na wenzio

Huo wivu wako wa sifa siku utachinjiwa baharini

Utasababisha samaki wakunyonye ulimi

Hivyo eeh bwana eeh utajiju

Kumbe mdomo ndio unaokufanya unachongachonga

Unakwenda nje ya mstari mpaka wazee wanasema unaboronga

Elewa wivu fitina vurugu zimemshinda bonga

Wamempiga juju kila siku anajifanya analonga

Ivi mnafikiri nini kukaa na kusema wenzenu

Mkuacha shughuli zenu mkaja mkaacha familia zenu

Mmeona hamna wa kusema mmeanza kusumbua wenzenu

Utajiju mi ni nani na nina asili ya nchi gani

Nikigundua we adui nakumiminia tu gun kitu gani

Dunia msumari wa moto shawambea usikuchome

La bongo mliache kama lilivyo la bush ndio hata usiliguse

We nyamaza kimya fikiria utawin vip

Ikiwa utajisahau familia yako itaishi vipi

Mdomo hamfanyi mtu kujisahau kwa fikra au kuishi kwa fitina

CHORUS

Usidhulu nafsi yako kwa kumsema mwenzio aliyetulia (aliyetulia)

Ukaipoteza time yako kwa kesi mbaya isiyo na sheria (sheria) X2

Kuyapinga mendeleo ya wenzio ni sawa na kukosa nidhamu kwa mwenzio (utajiju)

Kujifanya unajua na kubishia wenzio huku wewe unatega masikio (utajiju) X2

Lyrics Submitted by ambrozye8

Enjoy the lyrics !!!