DamnLyrics - The center provides all the lyrics

Wanamwabudu Nani? - Pst. Faustin S. Munishi



     
Page format: Left Center Right
Direct link:
BB code:
Embed:

Wanamwabudu Nani? Lyrics


Sikuyajua kama ndivyo yalivyo, mpaka roho aliponionyesha, shetani navyojua kujigeuza kama malaika yule wa nuru, mejigeuza makua rangi nyingi, mejiingiza kwa siri kanisani, watu wa Mungu wao bila kujua, ata wameanza kumuabudu, waraka wa yohana ule wa kwanza, sura ya tatu msitari wa nane, hazitendae dhambi ni wa shetani yeye alizitenda tokea mwanzo
Tunao watu wengi makanisani, kutenda dhambi kwao sio tishio, wakikutana pamoja kuabudu, swali mnijibu, wanamwabudu nani?
Kutoa pesa kwao sio tatizo, hawajaolewa waendelea kuzaa,hawajatubu dhambi wanazitenda, tena niviongozi wakina mama,hata kanisa wao ndo walojenga, wanadhamini mikutano ya nje, wakikutana pamoja kuabudu, swali mnijibu, wanamwabudu nani? Fungu la kumi kutoa siyo shida, lakini wameoa mabibi wengi, mchungaji kitaka kosana nao awaambie, watubu dhambi, gari la kanisa wao ndo linunua, napia vyombo kupazia sauti, wakikutana pamoja kuabudu, swali mnijibu, wanamwabudu nani?
Na wahubiri nao sio kidogo, niwashirika kumbe ni wake zao, wamewakuta watu wamesimama wanawaangusha wawaibie, wahubiri ujumbe wakutoa, wanasahau toba ya msamaha,wakikutana pamoja kuabudu, swali mnijibu, wanamwabudu nani? Na makanisa mengine ya ajabu,wokovu wa yesu wameukataa, kulewa pombe kwao sio ajabu, ata mchungaji anaibariki, ukiwaambia wewe umeokoka, wasema hiyo sio imani yao,wakikutana pamoja kuabudu, swali mnijibu, wanamwabudu nani?
Giza na nuru zinashirika gani, toeni giza katikati ya nuru, tumuabudu mungu mtakatifu, katika roho, na pia kweli, yesu ni kweli tena ndio uzima, na njia ya kutufikisha mbinguni, Mungu ataka sote tumuabudu katika roho na pia kweli, ewe shetani pepo uliomchafu nakuamuru kwa jina lake Yesu, toka nani ya kanisa lake Mungu uende kuzimu ukachomwe moto, tumegundua hila na njama zako, tukuabudu wewe ni kama nani?tunae Mungu wetu yehova, sifa utukufu ni wake milele
Lyrics Submitted by Sally Ombajo

Enjoy the lyrics !!!