DamnLyrics - The center provides all the lyrics

Yesu Ni Mzuri - Martha Mwaipaja



     
Page format: Left Center Right
Direct link:
BB code:
Embed:

Yesu Ni Mzuri Lyrics


YESU NI MZURI Lyrics By MARTHA MWAIPAJA
STARTING:heeeeh ni mzuri wewe BABA ni mzuri mno
CHORUS
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
VERSE 1:
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
wengi wameimba uzuri wako wewe na mimi kwa sehemu naweza imba
kuna wakati tunadhani tunaishi wenyewe tu kumbe MUNGU umeshikilia maisha yetu
ni mzuri wewe×2 wewe YESU wewe kwangu mimi ni mzuri tu
CHORUS
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
VERSE 2:
tunajivunia wewe kumbe wewe hulali husinzii BABA kwa ajili yetu usingetutoa pale tungeangamia hakika ule ulikuwa ni mwisho wetu akili zilishindwa maarifa yalishindikana usingetutoa BABA tungeangamia ni kweli wewe BABA usipoulinda mji alindaye akesha bure umepigana kwa waliopigana nasi umetuvusha katikati ya mtego
CHORUS
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe

VERSE 3:
Hapa ndipo tunajua thamani ya wokovu huu wokovu umetufanya tuwe salama asante BABA kwa kutuponya pale, wokovu huu BABA hatutauacha umetulinda leo umetutunza tena mioyoni mwetu BABA twakushukuru wokovu ni wa thamani wokovu ni wa thamani umetufanya tujue wewe YESU kuwa ni mzuri mno umetuponya tena umetulinda tena kwa moyo tunasema wewe ni mzuri mno si jambo rahisi sisi kuwa wazima tena ni wewe BABA umetuponya tena kwa kawaida hatuwezi simulia sana lakini wewe BABA umetuponya tena, leo tusingekuwepo tungeshasahaulika ewewe babababa umetupenda tena ni mzuri wewe ni mzuri wewe mioyoni mwetu twatambua wewe ni mzuri
CHORUS
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
ni mzuri wewe×2 YESU wewe ni mzuri wewe
Finishing:Ni mzuri wewe YESU,
umetukumbatia tena,ni mzuri wewe ,wetu wewe ni mzuri ,hatutakuacha yesu ,umetuokoa tena baba, ni mzuri wewe heee ni MZURI
Lyrics Submitted by Florence shoo

Enjoy the lyrics !!!