damnlyrics.com

Amebarikiwa

Amebarikiwa anyemtumaini Jehova Mungu Baba X2

Atakulisha atakunywesha kweli atakuvisha X2

Jamii yako yote itabarikiwa kamwe hutapungukiwa X2

Omba Jehova Mungu Wako kwa moyo wako wote atakupa ajaze moyo wako hatakuaibisha X2

Amebarikiwa anayetafuta uso wake Mungu Baba X2

Atakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua X2

Atakuponya atakufunulia ukweli na amani tele X2

Usichoke kutafuta uso wake Mungu Baba atakupa chochote utakacho yeye ni mwaminifu

Bwana anasikia maombi ya wenye haki atajibu Bwana hatawanyima kitu chochote

Amebarikiwa anayetafuta uso wake Mungu Baba X2

Atakufunika na mabawa yake Baba atakulinda X2

Atakuonyesha wokovu wake utaishi siku nyingi X2

Usichoke kutafuta uso wake Mungu Baba atakupa chochote utakacho yeye ni mwaminifu

Bwana anasikia maombi ya wenye haki atajibu Bwana hatawanyima kitu chochote X3

Enjoy the lyrics !!!