damnlyrics.com

Jipe Moyo

Dunia hii imejaa dhiki na vikwazo

Jipe moyo katika bwana×1

Dunia hii imejaa chuki na fitina

Jipe moyo katika bwana×1

Umesingiziwa jambo ambalo hujalifanya

Jipe moyo katika bwana×1

Umefutwa kazi hata bila sababu

Jipe moyo katika bwana×1

Jipe moyo

Jipe moyo

Bwana yesu amekuona×2

Kusoma umesoma lakini huna kaazi

Jipe moyo katika bwana

Kulima umelima lakini mavuno hakuna

Jipe moyo katika bwana

Moyo wako umejaa mafikira mengi sana

Jipe moyo katika bwana

Utakula nini,utavaa nini, utalala waapi

Jipe moyo katika bwana

Jipe moyo

Jipe moyo

Bwana yesu amekuona×2

Umekaribia harusi, mchumba wako amegeuka eeh

Jipe moyo katika bwana

Miezi tisa sasa mume wako hayuko nyumbani

Jipe moyo katika bwana

Jipe moyo maana mkombozi wako bado yuhai

Jipe moyo katika bwana

Usife moyo ndugu

Usife moyo dada

Jipe moyo katika bwana

Hujapata mtoto kwa miaka mingi sana

Jipe moyo katika bwana

Hata biashara zako zote zimefilisolisika

Jipe moyo katika bwana

Jipe moyo

Jipe moyo

Bwana yesu amekuonaaa×3

-jipe moyo-

Enjoy the lyrics !!!