DamnLyrics - The center provides all the lyrics

Liko Lango - Emachichi



     
Page format: Left Center Right
Direct link:
BB code:
Embed:

Liko Lango Lyrics


Liko lango moja wazi,
Ni lango la mbinguni,
Na wote waingiao,
Watapata nafasi.
Lango ndiye Yesu Bwana,
Wote waingie kwake,
Lango! lango,
La mbinguni ni wazi.
Yesu ndiye lango hili,
Hata sasa ni wazi,
Kwa wakubwa na wadogo,
Tajiri na maskini.
Hili ni lango la raha,
Ni lango la rehema,
Kila mtu apitaye,

Hana majonzi tena.
Tukipita lango hili,
Tutatua mizigo,
Tuliochukua kwanza,
Tutavikwa uzima.
Hima ndugu tuingie,
Lango halijafungungwa,
Likifungwa mara moja,
Halitafunguiwa.
Lyrics Submitted by MUTHONI MWITI

Enjoy the lyrics !!!