DamnLyrics - The center provides all the lyrics

Page format: Left Center Right
Direct link:
BB code:
Embed:

Juu Angani Lyrics

Nilipata bahati siku moja aaaha siku moja, kusafiri katika vyombo vile vipaavyo angani,
(juu juu angani)
juu juu angani panatisha panatia hofu na pia aah pana shangaza
(angani)
kuonesha uwezo kuwa mwenyezi Mungu yeyote aliyewahi fika huko atakuwa Shahidi
(juu juu angani)
juu juu angani panatisha panatia hofu na pia aah pana shangaza
(angani)
na wataalamu wa dunia wapaogopa hawana maelezo tosha kueleza wapaonayo.......
Huko juu kuna nafasi pana tena isiyokuwa na mipaka kwa macho waweza angalia hadi ukachoka iwe mashariki iwe magharibi kote ufanana aah hata kaskazini na kusini si rahisi kutofautisha
(juu juu angani)
juu juu angani panatisha panatia hofu na pia aah pana shangaza
(angani)
kuonesha uwezo kuwa mwenyezi Mungu yeyote aliyewahi fika huko atakuwa Shahidi
(juu juu angani)
juu juu angani panatisha panatia hofu na pia aah pana shangaza
(angani)

na wataalamu wa dunia wapaogopa hawana maelezo tosha kueleza wapaonayo.......
Vionekanavyo kwa macho ya watu hapo juu angani mawingu tuyaonayo huko juu yake pashangaaza sana
(juu ya mawingu tuonayo)
Mungu alipatandika tabaka la mawingu na juu ya hayo alitandika mawingu mengine
(angani)
wakati mmoja huwa yanazunguka na wakati mwingine hukaa sehemu moja na kutulia
(juu ya mawingu tuonayo)
Mungu alipatandika tabaka la mawingu na juu ya hayo alitandika mawingu mengine
(angani)
wakati mmoja huwa yanazunguka na wakati mwingine hukaa sehemu moja na kutulia
Huko juu ndege zipitako, juu yake pia kuna tabaka, hata waatalamu wa dunia hawajui mwisho wake hapo juu ya juu ya juu huko ndiko Mungu aliko Jalali ameketi juu mbinguni Mungu wetu wa heshima
(juu juu angani)
watakatifu watapaa na wataruka hawatahitaji ndege wala roketi wao ni kupaa tu
(siku hiyo)
ndipo watakapo funuliwa siri zote wafafanuliwe kuhusu nguvu tuonazo angani
(juu juu angani)
watakatifu tutapaa na tutaruka hatutahitaji ndege wala roketi sisi ni kupaa tu
(siku hiyo)
ndipo tutakapo funuliwa siri zote tufafanuliwe kuhusu nguvu tuonazo angani
(juu juu angani)
watakatifu watapaa na wataruka hawatahitaji ndege wala roketi wao ni kupaa tu
(siku hiyo)
ndipo watakapo funuliwa siri zote wafafanuliwe kuhusu nguvu tuonazo angani
(juu juu angani)
watakatifu tutapaa na tutaruka hatutahitaji ndege wala roketi sisi ni kupaa tu
(siku hiyo)
ndipo tutakapo funuliwa siri zote tufafanuliwe kuhusu nguvu tuonazo angani......
Lyrics Submitted by Ian Kigen (bossbaby)

Enjoy the lyrics !!!