Kuna Siku - Ambassadors Of Christ Choir
| Page format: |
Kuna Siku Lyrics
Kuna siku,iliyo kuu,
'Tasubiri,ikaribu
Ndiyo siku,siri zetu
Zitafichuliwa,
kila tendo ulotenda,
Liwe jema au baya,
Siku hiyo,ndugu yangu,
Litawekwa wazi
Siku hiyo ndugu ni siku ya kutisha,
Kwa wale wote walio ukataa wokovu,
Tena siku hiyo ni siku ya furaha,
kwa wale wote walio mpokea mwokozi
Kila jina siku hiyo litaitwa
Na matendo yako yote yataletwa
Utajibu ninii,nitajibu ninii
Mbele ya mahakama iliyo kuu
Mungu mwenyewe akiwa ndiye hakimu
Utajibu ninii,utajibu ninii
Siyo mbali ndugu zangu
Dalili zote zinaonyeha
Mwisho wa mambo yote U karibu
Yachunguze matendo yako,
Ufanye uamuzi leo
Mambo ya kesho huyajui
Njoooo×2
Bado kitambo tuu
Yapaswa kujitakasa
Siku hiyo ikifika
Tuwe tumetakasika
Mwokozi Yesu akija
Tumlaki kwa furaha
Karibu sana mwokozi
Njoo utuokoe
Bahari na milima vitamkimbia
Akija na utukufu wa Babye
Je!utasimama,au utakimbia?
Lakini wateule wote siku hiyo
Walio andikwa kitabu cha uzima
Watarukaruka,nami nitaruka
Siyo mbali ndugu zangu
Dalili zote zinaonyesha
Mwisho wa mambo yote U karibu
Yachumguze matendo yako
Ufanye uamuzi leo
Mambo ya kesho huyajui,
Njooo×2
Kila jina siku hiyo litaitwa
Na matendo yako yote yataletwa
Utajibu nini,Nitajibu nini
Mbele ya mahakama iliyo kuu
Mungu mwenyewe akiwa ndiye hakimu
Utajibu nini,uitajibu nini
Bahari na milima vitamkimbia
Akija na utukufu wa Babaye
Je! Utasimma,au utakimbia
Lakini wateule wake siku hiyo
Walioandikwa kitabu cha uzima
Watarukaruka,nami nitaruka
Siyo mbali ndugu zangu
Dalili zote zinaonyesha
Mwisho wa mambo yote U karibu
Yachunguze matendo yako
Ufanye uamuzi leo
Mambo ya kesho hyajui
Njooo×2
Lyrics Submitted by Kelvinabuti