Kekundu - AIC Makongoro Vijana Choir
| Page format: |
Kekundu Lyrics
[INTRODUCTION STANZA]
Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa
Tena ni jambo lenye thamani
Bali wapumpavu huidharau hekima hii wanahangaika
Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa
Tena ni jambo lenye thamani.
[PRE CHORUS]
Ooh wajinga ndio waliwao (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao mama (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao.
(STANZA 1)
Mtu mmoja alilipwa malipo ya uzeeni , akafurahi Sana
Wakati anarudi nyumbani kwake alikutana na jeshi la Shetani
Wakamwambia lete pesa tuizalishe uwe na pesa nyingi nae pasipo kufikiri kwa Nini hawa wasizalishe zao
Aliwahesabia pesa zote
Matapeli nao wakamwacha pekee
Alisubiri akachoka , mwishowe akagundua
Amekwisha ibiwa
(CHORUS)
Kekundu kekundu (kekundu)
Kekundu kekundu (kekundu)x2
[PRE CHORUS]
Ooh wajinga ndio waliwao (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao mama (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao.
(STANZA 2)
Alikuwepo mama mmoja
Alitafuta dawa apendwe na mmewe
Alileta mizizi hiyo nyumbani
Na kumwekea mmewe kwenye chai
Tumaini la mama yule
Mmewe Sasa atampenda Sana
Laiti Kama angejua kuwa
Upendo unatoka kwa Yesu
Usiku ulifika Bwana yule akawa tabani
Mpaka akakata roho
Mama yule aligundua kuwa
Haikuwa dawa , ilikuwa ni sumu.
(CHORUS)
Kekundu kekundu (kekundu)
Kekundu kekundu (kekundu)x2
[PRE CHORUS]
Ooh wajinga ndio waliwao (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao mama (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao.
(STANZA 3)
Mtu mwingine na uzombi wake alinichanganya
Kupigiwa ramli aliketishwa
Katika kigoda na elimu take
Akitaka ukubwa
Na kwa kuwa moyoni mwake Yesu hayupo
Hakujua chochote
Laiti Kama angejua
Mganga wake hata shule hakwenda
Alilipa pesa kisha akavalishwa ilizi kubwa
Eti apande cheo
Matokeo akafukuzwa kazi siku sio nyingi
Mambo yaligeuka
(CHORUS)
Kekundu kekundu (kekundu)
Kekundu kekundu (kekundu)x2
Shetani kekundu (kekundu).
[PRE CHORUS]
Ooh wajinga ndio waliwao (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao mama (wajinga ndio waliwao)
Ooh wajinga ndio waliwao.
(STANZA 4)
Binti mmoja Alidhani yakuwa kapata
Kumbe kapatikana
Alikataa wachumba wengi
Waliokuja kuposa eti ni maskini
Hayawi hayawi yakawa
Alimpata aliyemtafuta
Alimpata mwenye pesa wakaoana
Maisha yakaanza
Vituko vilianza kupishana siku hata siku
Mambo yaligeuka
Dada yule aliona ni afadhali aliyekufa
Asiutese moyo
Kekundu sipende pesa (kekundu)
Kekundu kekundu (kekundu)
Kekundu kekundu (kekundu)x2
[CONCLUDING STANZA]
Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa
Tena ni jambo lenye thamani
Bali wapumpavu huidharau hekima hii wanahangaika
Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa
Tena ni jambo lenye thamani.
BY CARLIN OSCAR KIKOYO
[email protected]
Tell No: 0692893425
Lyrics Submitted by Carlin Oscar Kikoyo