Mahangaiko - Ushirika Morovian Choir
| Page format: |
Mahangaiko Lyrics
Mahangaiko yakizidi,
Unanifariji,
Moyo wangu ukilemewa,
Wanifurahisha,
Hata ninapoteleza,
Wewe mwenyezi Mungu,
Hautanitelekeza,
Wala hauniachi ndiyo maana nakuhitaji,
Kila wakati
Mambo yanapoteteleka,
Hukawii,
Mara moja unapotea
Unakata Kati,
(Chorus)
Hata ninapojisahau,
Wanigusa,
Wanifichua nirejee
Kwenye mstari
(Chorus)
Nikavamiwa na adui,
Huchelewi,
Haraka wanapigania,
Unanitetea
(Chorus)
Nikiomba waniskia,
Wanijibu,
Wewe Ni mwema wa ajabu,
Ni mkarimu
(Chorus)
Nataka Nione uso wako,
Kila wakati
Na nikiamka niamke nishibishwe,
Kwa sura yako,
Sigeuki nyuma sitafuti,
Mungu mwingine,
Kwani wewe hujawai kuniwacha,
Pekeyangu,
Na ndiyo maana nakuhitaji,
Kila siku
Na ndiyo maana nakukabidhi,
Kila kitu,
Na ndiyo maana nakuhitaji,
Kila wakati,
Na ndiyo maana nakuhitaji,
Kila siku,
Na ndiyo maana nakukabidhi,
Kila kitu,
Na ndiyo maana nakuhitaji,
Kila wakati