Mrema - Remmy Ongala
| Page format: |
Mrema Lyrics
Mrema aaa mrema (Mrema oo)
Mrema aaa mrema (Mrema wee)
Mrema aaa mrema (Murema)
Mrema aaa mrema (utuokoe)
Mrema aaa mrema (Mrema wee)
Mrema aaa mrema (Madhambi yote)
Mrema aaa mrema (Jamani mrema)
Mrema aaa mrema
Eeee..
Lamgambo limelia ×2
Tumetangaza vita dhidi ya wala rushwa wafanyaji magendo walanguzi wasiowajibika
Na wale wanaohujumu uchumi wa taifa
Mrema huyooooo...
Wengine wanalalamika eti mrema kawaingilia
Wengine wanasema mrema kavuka mipaka
Ni mipaka gani hioo ndani ya hii nchii
Mrema huyooo
Anawasaka
Pembe hadi pembe
Anawasaka
Kona hadi kona
Anawasaka
Mpaka nyarugusu
Hadi kule mpanda
Mpaka kule chunya
Uwanja wa mdege.
Wengine wanalalamika eti mrema kawaingilia
Wengine wanasema mrema kavuka mipaka
Ni mipaka gani hioo
Tunakujua wewe ni mwizi
Tunakujua Unaua tembo
Tunakujua unauza pembe
Tunakujua wewe ni jambazi
Mrema huyoooooo
Ubaya tumeukaribisha wenyewe ×2
Sasa tunabaki tunalaumiana wenyewe
Sasa tunabaki tunatukanana ee.
Wee unajua huyu fundi viatu eti mnamchagua mwenyekiti wa CCM
(Sheria za chama atajua kweli- hajui)
(Kwanza hata kuandika jina lake -hajui , sanasana uchawi)
Wasomi wanakufa na majungu.
Ubaya tumeukaribisha wenyewe
We unajua huyu mwanajeshi
eti unampeleka kwenye FAT Sheria za mpira atajua kweli - hajui.
Na matokeo yake ee
rufaa baada ya rufaa juu ya rufaa - he hee mambo.
Serikali imeibiwa milion 4
Tume ya uchunguzi inatumia 12
Na huo ni wizi ndani ya serikali(juu ya wizi)
Police wapo, mahakama zipo, vyombo vya sheria vipo,Tume ya uchunguzi kwanini?
Wale mapolice hawana vyeo
Akimkamata mwaribifu akifika kwa mwenye cheo kesho anaachiliwa
Kesho atamkamata tena(hapana)
Atachukuq rushwa.
Mrema fika kariakoo
Mrema nakushauri fika mwanza ee
Mwarabu na pajero (he hee)
Wasukuma na baiskeli(maskinii)
Dhahabu wanachimba wenyewe
Almasi wanachimba wenyewe
Pamba wanalima wenyewe
(He heee hatari.)
Mrema ukifika mwanza ee
Usisahau kufika makoroboi.
Wavuja jasho( ee)jua kali (he heee wamo tuu)
Huko kwa wanyongee
Mrema fika Nyarugusu, fika bokoli ,fika rugusu
(Sangara)
Sangara kwa wingi
Hata sangara wanaibiwa ee (jamanii)
Mrema tazama muharibifu
Wala usimuonee aibu mrema
(Kazi moja)
Mrema rungu lao
...malisela , Mwinyi hataki mchezo
Wale waliokuwa wanamwimbia Nyerere
Nyerere amewaacha kwenye mataa
(Muraa....)
Lyrics Submitted by Sway