Nipo Katikati - Kwaya Mt Maria Karatu
| Page format: |
Nipo Katikati Lyrics
IMANI YANGU
Niko katikati ya mbingu na ardhi,
Ninaning’inia sina pa kushika
Duniani sipo na mbinguni sipo
Ninawayawaya Bwana niokoe
/s/ Nikienda huku mambo moto moto
Nikienda kule ni baridi tupu
Mbele yangu giza, nyumba yangu giza
Mahubiri mengi yananiyumbisha imani
/a/ kumtafuta Mwokozi
Ee Mungu wangu uko wapi, ili nije kwako hima,
Mbele yangu kuna giza nene, na nyuma yangu
ni giza, mahubiri mengi yamezidi
Na mengine yananiyumbisha imani
/t/ Nikienda huku ninabatizwa na
nikirudi (kule) ninaitwa mimi kafiri
Giza pande zote mahubiri ni mengi
Na mengine yananiyumbisha imani
/b/ nikienda huku ni moto nikirudi huku baridi
Vuguvugu haitakiwi na imani yangu yayumba
Mungu wangu nisaidie niokoe nisipotee
Mahubiri mengi
Na mengine yananiyumbisha imani
Manabii wengi wananiyumbisha,
Nifuate yupi nimuache yupi
Wapo wa uongo, wapo wa kweli,
Njoo Bwana Yesu Rudi kwetu hima
Ulimwengu huu ulioufia umekuwa Jela la maskini
Roho yangu Bwana inakutamani
wewe peke yako ndiwe tiba yangu
neno lako Bwana litaniponya
Kwa sababu wewe Mungu ni mmoja
Twakuomba Baba utuunganishe
Matabaka yote na yatoweke
Lyrics Submitted by allan massawe