damnlyrics.com

Shilingi Yaua Tena Maua

Shilingi Yauwa Tena Mauwa

Ama kweli dunia ooh dunia

Ooh wake kwa waume

Baba ooh twasumbuka

Enzi ya Adamu na Eva

Dunia ilikuwa nzuri

Enzi ya Adamu na Eva

Dunia ilikuwa nzuri iyaah

Lakini dunia ya leo

Bila kuwa na pesa

Hakuna sauti mama

Ooh kusikika iyaah

Iwe mwanamke au iwe mtoto

Iwe mzee kila mtu mawazo yake mikopo

Aah Stella

Sasa ninashangaa ninapoona dunia

Kila mtu yuko mbio kutafuta shilingi

Kila mtu yuko mbio kutafuta shilingi iyaa

Hata ukiona hapo *Mbindo anapohangaika

Mawazo yake yote yako kwa shilingi iyaa

Uwe na sura nzuri baba ya kupendeza

Kama huna shilingi mambo yako ni bure iyaa

Mapenzi ya zamani yalikuwa ni bure

Zamani za kale mambo yalikuwa shwari

Lakini kisirani shilingi baba ikaharibu

Sasa hakuna cha bure dunia baba ni shilingi

Hata mtoto mchanga yule aliyezaliwa leo

Anapolia mama eeh mama eeh mama

Hebu tupa shling pale atakuonyesha pengo

Ama kweli shilingi ni sabuni ya roho

Hata kama una mawazo shilingi itakusafisha roho

Aah jamani

Hata yule mnyama yule wa siku hizi

Hebu tupa shilingi pale pale baba atakurarua

Iwe mzee wa miaka baba hamsini

Bora awe na shilingi warembo watamwandama

Na wewe kijana utaachwa hapo hapo iyaa

Ooh jamani

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi ni tamu baba usiidharau

Hiyo shilingi moja inaweza kuvunja mlima

Hiyo shilingi moja inaweza ulale pakubwa

Usidharau shilingi baba yaua

Mama ooh ooh

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Katikati ya mapenzi bila shilingi ni bure

Weye useme yote bila mapesa ni ngumu

Hata uwe na sura ya kupendeza baba ni ngumu

Bora uwe na shilingi mambo yako yatanyooka

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi itakufanya weye baba uimbe

Tena shilingi itakufanya uwe ofisa

Hata ukiwa na miaka ishirini na tano baba

Pale pale utaitwa mzee

Pale pale utaitwa mzee wa shilingi

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua yeeh

Ooh

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Hakika shilingi ni kitu baba bora

Hiyo shilingi moja itakufanya baba usipande basi

Usidharau shilingi baba yang’ara

Katikati ya roho binadamu baba yang’ara iyee

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua eeh

Ukitaka chochote dunia baba ni shilingi

Ukiwa na mpenzi wako ooh maneno tupu

Hayavunji mfupi wewe bwaga shilingi mezani

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Mambo yafike magumu hayapitiki

Kati ya mapenzi hata useme mazuri

Lakini ukiona mwanamke anapita vile na vile

Weye toa shilingi juu weye utakubaliwa sana

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua

Shilingi yaua ooh tena maua iyaah aah

Lyrics Submitted by Trust Jeferson

Enjoy the lyrics !!!